ADHANA FM DIGITAL
ADHANA FM DIGITAL
7 July 2024, 7:06 am
Na Juma Haji Adhana FM.
Mbunge Wa Jimbo La Chaani Juma Usonge ameishauri Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa waskazini Unguja kutatua changamoto za wakulima wa bonde la mpunga Kibokwa ili kufikia lengo la serikali kupitia sekta ya Kilimo hapa nchini.
Ameyasema hayo katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kaskazini Unguja kilichofanyika Mahonda katika Ofisi za chama hicho kwa lengo la kusikiliza utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imefanywa na serikali.
Aidha amewashauri viongozi wanaosimamia Sekta ya kilimo kufanya utafiti wa mabondea ya kilimo ili kufahamu aina ya kilimo kinachotakiwa kulimwa katika maeneo hayo jambo ambalo litakalosadia kuleta mapinduzi ya kilimo kwa wakulima.