Adhana FM

Baraza la Biashara Kaskazini Unguja lahimizwa kushirikiana na wafanyabiashara

7 May 2024, 8:13 pm

Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Rashid Hadidi Rashid  amelishauri Baraza la  biashara la mkoa huo kushirikiana na  wafanyabiashara ili kukuza pato la taifa.

Na Abdul-Sakaza na Juma Haji, Kaskazini Unguja

Rashid ameyasema hayo  leo ofisini kwake Mkokotoni wakati alipokutana na baraza la biashara la mkoa huo katika mkutano wa kutathimini na kujadili maendeleo ya bishara Kaskazini Unguja.
Amesema baraza la biashara ni chombo  muhimu cha kuwaunganisha wafanya biashara ili kukuza uchumi katika mikoa na nchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewasihi wafanya biashara kuacha kukwepa kodi na amewahimiza kukata vibali vya biashara ili kuondoa usumbufu wakati wanapoendesha biashara zao.

Nao wajumbe wa biashara wa mkoa huo wamesema wanaendelea kushirikiana na wafanyabiashara na pia wako tayari kutoa elimu kwa walengwa ili kufikia lengo.

Kikao hicho ni muendelezo wa mikakati ya nkoa wa kaskazini Unguja kikiwa na lengo la kuweka mazingira salama kwa wafanyabiashara na kuhakikisha wanatimiza matakwa ya kisheria ikiwa ni pamoja na wanalipa kodi kwa wakati.