Adhana FM

Baraza la Mji Kaskazini A kupunguza msongamano wa wafanyabiashara Soko la Kinyasini

7 August 2023, 10:30 am

Afisa mipango miji wilaya Kaskazini A, Meya Ali Moh’d akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu mpango wa kuwapanga wafanyabishara wa soko la Kinyasini Unguja. Picha na Juma Haji wa Adhana FM.

Ujenzi wa masoko unavyochangia kuondoa msongamano wa wafanyabiashara katika nchi yetu.

Na Juma Haji Juma

Baraza la mji Wilaya ya kaskazini A Unguja linakusudia kuondosha msongomano wa wafanyabiashara wa soko la kinyasini kwa kujenga masoko mawili makubwa yatakayotoa fursa kwa wananchi kuendeleza biashara zao.

Akizungumza na Adhana  FM Afisa mipango miji wa Baraza la mji Wilaya ya kaskazini “A” Unguja Meya Ali Moh’d amesema pamoja masoko yakokuwepo , bado kuna  chaangamoto zinazotatiza  ufanisi wa utendaji kazi kwa baadhi ya wafanyabiashara kutokana na ufinyu wa nafasi unaosababisha msongamano.

Amesema njia pekee ya kutatua changamoto hiyo inayopelekea baadhi ya wafanyabiashara kuuza bidhaa barabarani na sehemu zisizoruhusiwa ni kujenga masoko makubwa katika eneo la kinyasini na mkwajuni.

Aidha Bi Meya aesema kuwa, kukamilika kwa masoko hayo kutapunguza mrundikano wa wafanyabishara na hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kufuata huduma kwenye maeneo ya karibu.

Nae Yussuf Mgeni Ramadhan mjasiriamali kutoka Mkokotoni anayefanya shughuli zake katika soko la Kinyasini, ameIpongeza baraza la mji Kaskazini “A” kwa hatua zinazochukuliwa na uongozi katika kuwasogezea karibu fursa za kiuchumi zinazojitokeza katika Mkoa huo.