Adhana FM

SMZ imeombwa kutenga eneo maalum kwa wajasiriamali kuekeza

28 September 2021, 10:35 am

Wanavikundi vya federation Zanzibar wakishriki mkutano wa wajasiriamali

Na Ali Khamis, Wilaya ya Magharib B

Shirika la Centre for Community Initiaties (CCI) Tanzania  limetoa pendekezo kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kutoa eneo  maalumu la kiuchumi litalotumika kuwekeza viwanda vidogo kwa vikundi vya wajasiriamali wa hali ya chini.

Mkurugenzi wa CCI, Timothy P Ndezi ametoa ombi hilo huko Kinuni Magaharib B  kwenye ziara ya kuangalia changamoto zinazozinaukabili muungano wa vikundi vya Tanzania Urban Poor Federation kwa upande wa Zanzibar

Sheha wa shehiya ya Kinuni amewahimiza wananchi wa shehiya nyengine za Unguja an Pemba kuupokea muungano wa vikundi vya federation ili mujikwamua na umasikini.

Naye katibu wa kikundi cha Tumejipanga cha Kinuni amesemavikundi vya federation vinasaidia sana wanawake  katika harakati zao za maisha ya kila siku ikiwemo kikidhi mahitaji ya nhumbani na elimu kwa watoto wao.

Akifafanua kuhusu muungano huo Mratibu wa Vikundi vya Feederation Zanzibar, Sadifa Othman amasema mtu akijiunga na muungano wa huo huamka kimawazo katika kufanya shughuli za miradi ya kiuchumi

Zanzibar ina jumla ya vikundi 32 vya muungano wa Federation katika mkoa wa Mjini Magharib na Kasakazini Unguja  ambavyo mbali na kujiwekea akiba,wanachama wake wanafanya ujasiriamali wa  bidhaa mbali mbali ikiwemo ushoni wa nguo na mashuka, kutengeneza sabuni, dawa za kusafishia vyoo pamoja na ususi wa mikoba.