Triple A FM
Triple A FM
18 July 2025, 9:38 am

“Hatuwezi kuendelea na vichekesho lazima taaluma iwe serious…Vichekesho vilikuwa vinachukua nafasi kubwa kuliko uandishi wa habari”
Na Anthony Masai
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amevimwagia sifa vituo vya redio za kijamii nchini vilivyo chini ya mwamvuli wa TADIO na kueleza kuwa vinafanya vizuri katika ukusanyaji, uchakataji na utoaji wa habari zenye usahihi.
Balile ameyasema hayo mkoani Arusha katika mahojiano aliyoyafanya na redio Triple A kuhusu umuhimu wa TADIO kwa jamii pamoja na suala la waandishi wa habari kujisajili kwenye Bodi ya Ithibati.
Amesema bado redio jamii zinaaminika pakubwa na wananchi kutokana na kuwa karibu nao zaidi.
Akizungumzia usajili wa waandishi wa habari kwenye Bodi ya Ithibati amewataka waandishi ambao hawajakidhi vigezo kuhakikisha wanafuata sheria kwa kutafuta vigezo vinavyotakiwa ili wanedelee kuihudumia jamii.
Vilevile amewakumbusha wanahabari kuwa makini katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi mkuu na kuamua kufanya jambo moja kwa wakati ikiwamo kusimama uandishi kwa muda ili kugombea ikiwa ana uhitaji hali ambayo ittapunguza mgongano kwenye wa taaluma na siasa.