Ruangwa FM

Mfumo dume watajwa kuwanyima wanawake nguvu katika mapato ya korosho

20 September 2026, 22:24

Picha Miti ya korosho.

Licha ya wanawake kuwa sehemu muhimu ya nguvu kazi katika uzalishaji wa korosho, takwimu za usajili mkoani Lindi hadi Septemba 2026 zinaonesha wanaume bado wanaongoza katika umiliki wa mashamba ya zao hilo.

Na Loveness Daniel.

Mfumo dume umetajwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazoweza kuwafanya wanawake kutonufaika kwa usawa na mapato yatokanayo na zao la korosho, licha ya kushiriki katika hatua mbalimbali za uzalishaji.

Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Brigedia Mstaafu Damian Mwanjile, amesema wanawake wanapaswa kuhakikisha wanamiliki na kusajili mashamba ya korosho kwa majina yao, ili kuimarisha nafasi yao katika kufanya maamuzi na kunufaika na mapato yatokanayo na zao hilo.

Mwenyekiti Bodi ya Korosho Damiani Mwanjile.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Ruangwa FM wameeleza kuwa bado kuna changamoto katika baadhi ya familia, ambapo wanawake hushiriki kwa kiasi kikubwa katika shughuli za uzalishaji wa korosho, lakini hawashirikishwi kwa kiwango sawa katika maamuzi kuhusu matumizi ya mapato yanayotokana na zao hilo.

Sauti za wananchi.

Takwimu za Taarifa za Usajili wa Wakulima Mkoa wa Lindi hadi tarehe 18 Septemba 2026 zinaonesha kuwa jumla ya wakulima 173,080 wamesajiliwa, ambapo wanaume ni 104,114, sawa na asilimia 60.2, huku wanawake wakiwa 68,966, sawa na asilimia 39.8.

Kwa upande wake Abdalah Nampapuka Kiongonzi kutoka Rweje AMCOS amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu usawa katika mapato ya korosho, hatua inayolenga kupunguza huku akisema changamoto hiyo kwa Sasa inapungua.

Abdallah Nampapuka Makamu Mwenyekiti , Rweje AMCOS.