Ruangwa FM

Acheni kutumia madawa ya kulevya – DC. Mgandilwa

16 April 2021, 7:23 am

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, MH. HASHIM MGANDILWA, amewataka vijana wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi mdogo wa madini ya dhahabu Njawale uliopo katika kijiji cha Mibure wilayani humo, kuacha tabia ya kutumia madawa ya kulevya na kununua wanawake ambao wamekua na kawaida ya kujitokeza katika maeneo mbali mbali ya machimbo na kubainisha kuwa kujihusisha na masuala hayo kutapoteza nguvu kazi ya Taifa.

Mgandilwa ameyasema hayo alipotembelea katika mgodi huo mpya ambao uliibuka march 17 mwaka huu kwa kutoa madini ya dhahabu, ambapo alifika na timu ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ili kutoa elimu ya usalama katika mazingira ya mgodi ili kuepukana na ajali ambazo zimekua zikitoke katika maeneo mengi ya machimbo hasa ya kufukiwa na kifusi hususan kwa nyakati hizi ambazo mvua zimekua zikiendelea kunyesha nchini kote, ambapo pamoja na elimu hiyo akagusia masuala ya umuhimu wa vijana hao kutunza afya zao wakiwa katika shuguli zao za uchimbaji.