Ruangwa FM

Ruangwa wazindua zoezi la chanjo ya surua, rubela

15 February 2024, 10:28 pm

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mh Hassan Ngoma amezindua rasmi zoezi la chanjo ya surua rasmi Leo tarehe 15/2/2024 wilayani Ruangwa.
Dc Ngoma amewaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kutumia nguvu ileile waliotumia wazee kuitokomeza surua kwani ni ugonjwa huo ni hatari unaosababisha ulemavu hivyo wananchi wameombwa kutoruhusu ugonjwa huo kurejea kwenye familia zetu.

Nae mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian chonya amesema wao kama halimashauri wamejipanga na taratibu zote zimekamilika na dhamira yao ni kuchanja Kwa asilimia miamoja ikibidi zaidi nakumuahidi mkuu wawilaya watafika kote ikiwemo mipakani mwa wilaya kwani chanjo hii hailengi wanaokaa mijini pekee.

Kwaupande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Ruangwa Dr Feisal Said amesema chanjo ya surua na rubela walengwa ni watoto chini ya miaka mitano lengo nikuwatengenezea Kinga dhidi ya ugonjwa wa surua na rubela, huku lengo nikuchanja zaidi ya watoto 17,242, lakini pia huduma hizo zitatolewa sehemu muhimu kama vile mashuleni,kwenye mikusanyiko pia Kuna chanjo mkoba na chanjo tembezi, hivyo amewaasa wananchi wajitokeze Kwa wingi.