Ruangwa FM

Unywaji wa maziwa sio tiba ya kifua kikuu (tb) wala ya kusafisha koo kwa ajili ya vumbi

23 March 2023, 7:05 pm

Na Loveness Daniely

Wachimbaji wadogo wa madini namungo wilaya ya ruangwa wakipewa elimu juu ya ugonjwa wa TB.

Unywaji wa maziwa watajwa kua sio tiba wala haiwezi kuzuia kifua kikuu TB  au kusafisha vumbi kifuani  bali unywaji wa maziwa huimarisha kinga ya mwili kwakua maziwa yana virutubisho vingi mwilini  vyenye kuujenga mwili na kuimarisha mwili katika kupambana na maradhi tofauti na dhana katika jamii nyingi zinavyozania .

Hayo yamebainishwa na mshauri wa wa magonjwa ya TB,Ukoma na ukimwi kupitia mradi wa USAID Afya yangu mkoa wa lindi Dr.Jamila Kassim  leo march 23 katika kijiji cha namungo wilayani Ruangwa walipotembelea wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa namungo wakitoa elimu juu ya ugonjwa wa kifua kikuu na upimaji wa ugonjwa kwa wenye dalili za TB.

Sauti ya Mshauri TB,ukoma na Ukimwi mkoa wa lindi

Mchenjuaji wa madini aliyejitambulisha kwa jina la Othman Mussa akiuliza swali kwa madaktar hao ameda kua wao kama wachimbaji wamekua wakitumia maziwa kuepuka kupata maambukizi ya mapafu na kifua kikuu kwani kazi yao inawapa hatari ya kupata maambukizi kutokana na vumbi,

‘’Je doctor ni sahihi tunavyokunywa maziwa kua tunasafisha vumbi na tunaweza kujikinga na TB  kama ilivyo mtazamo katika jamii zetu’’?Othimani Musa amesema

‘’Je doctor ni sahihi tunavyokunywa maziwa kua tunasafisha vumbi na tunaweza kujikinga na TB  kama ilivyo mtazamo katika jamii zetu’’?Othimani Musa amesema

Hata hivyo baadhi ya wachimbaji wameomba serikali kuwatembelea walau kwa mwezi mara moja kwani waliowengi wachimbaji imekua ugumu kufika katika vituo vya afya kutokana na shughuli zao za kila siku ambazo kwao ni risk kutokana na wakati mwengine kukosa hewa ya kutosha pamoja na vumbi maeneo ya mgodini.

Madaktari bingwa wa kupima na kutoa elimu juu ya ugonjwa wa kifua kikuu wapo wilaya ya ruangwa katika maadhimisho ya wiki ya kifua kikuu ambayo inaadhimishwa kimkoa katika wilaya ya ruangwa  itakayofanyika 24 march yenye kauli mbiu ‘’Okoa Maisha wekeza kutokomeza kifua kikuu Nchini”

sauti za wananchi Namungo