Ruangwa FM

CBT yawanoa VEOs, maafisa ugani, makarani kidigtali zaidi

15 February 2024, 8:49 pm

Bodi ya Korosho Tanzania CBT yatoa mafunzo ya uhuishaji na usajili mpya wa wakulima pamoja na taarifa zao katika zao la korosho ili wakulima kupata mgao sahihi wa pembejeo za kilimo katika zao hilo kuendana na kusudio la serikali.

Kaimu Meneja Bodi ya Korosho Humphrey Mlagalila tawi la Lindi amesema lengo la mafunzo hayo ni kila mkulima apate kinachostahili katika ugawaji wa pembejeo. Hata hivyo awali kulikuwa na mkanganyiko wa taarifa za wakulima hivyo mafunzo yamelenga idadi ya mashamba, ukubwa wa shamba, jumla ya mikorosho aliyonayo mkulima pamoja na utambulisho wa mkulima.

Mafunzo hayo yametolewa leo 15 Februari 2024 katika ukumbi wa chuo cha Veta Nandagala wilayani Ruangwa ambayo yamehusisha maafisa ugani, makarani waliochaguliwa pamoja na watendaji wa vijiji na mafunzo hayo yamefanyika kila tarafa wilayani hapa.

Sauti ya kaimu manager humphrey.

Afisa ugani kata ya Nandagala Zaituni Natunga amesema uwezeshwaji wa mafunzo hayo ni chanzo cha kuongeza mapato katika wilaya kwani watendaji watafahamu wakulima wao na idadi halisi ya mashamba ya mikorosho wanayomiliki pia kulingana na taatifa hizo ambazo zitatambua upimaji wa mashamba kidigtal wakulima watazingatia kilimo bora.

Pia Thomasi Mandondo ni mmojawapo wa makarani aliyehudhuria mafunzo hayo ameipongeza Bodi ya Korosho Tanzania kwa kuwajali wakulima kwani taarifa zao sasa zitahifadhiwa kidigtali hivyo serikali kujua hali halisi ya wakulima na kuwasaidiwa katika pembejeo za kilimo.