Ruangwa FM

Tutatumia sheria kwa wazazi wasiopeleka watoto shule

3 February 2023, 7:10 pm

Na Loveness Daniely.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi Hassan Ngoma   amesema kuanzia February 6 2023 wataanza kufanya msako mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba kwa kutumia sharia na miongozo iliyopo  kwa wazazi wasio wapeleka Watoto shuleni msako huo ni ili kubaini watoto ambao hawajaripoti shuleni kwa wale waliofaulu kuingia kidato cha kwanza pamoja na watoto waliofika umri wa kuanza darasa la kwanza na awali. 

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa MH. HASSAN NGOMA akiongea na wazazi walezi na wanafunzi. Picha na Joshua Jeremiah

Ngoma ameyasema hayo leo alipokuwa anazungumza na Ruangwa fm Radio ofisini kwake wakati akibainisha hatua zinazoendelea kuchukuliwa kwa wazazi wasiowapeleka watoto wao shuleni huku akibainisha kuwa kwa sasa wanaendelea kufanya ziara katika kata mbali mbali za Wilaya  ambapo mpaka hivi sasa tayari wameshazungumza na wazazi na walezi katika kata 12 kati ya kata 20  ambapo matarajio ni mnamo kufikia mpaka jumamosi ya February 4  watakuwa wamekamilisha kwa kata 8 zilizosalia .

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa akizungumza hatua zitakazochukuliwa kwa wazazi wasiopeleka watoto shule

Akizungumzia hali ya uandikishwaji wa wanafunzi kwa madarasa ya awali na la kwanza Afisa Elimu awali na Msingi halmashauri yawilaya ya Ruangwa mwalimu George Mbesigwe amesema mpaka sasa halmashauri hiyo wamevuka lengo la maoteo ya uandikishaji wa wanafunzi ambapo mpaka sasa wameshafika asilimia 117 % 

“Kwa mwaka wa masomo 2023 halimashauri iliotea kuandikisha wanafunzi wa awali 3367 , wavulana 1664 na wasichana 1703 ambapo mpaka February 02/2023 tayari wameandikisha wanafunzi 4087 ambao wavulana 2068 na wasichana 2019 sawa na asilimia 121%.”Amesema Mbesigwa.

“Kwa mwaka wa masomo 2023 halimashauri iliotea kuandikisha wanafunzi wa awali 3367 , wavulana 1664 na wasichana 1703 ambapo mpaka February 02/2023 tayari tumeandikisha wanafunzi 4087 ambao wavulana 2068 na wasichana 2019 sawa na asilimia 121%.”Amesema Mbesigwa

Hata hivyo Mbesigwe amesema zipo sababu mbali mbali zilizopelekea uandikishwaji wa wanafunzi hao kupanda ambapo ni pamoja na mabadililoko ya uandikishaji wa wanafunzi ambapo miaka ya nyuma uandikishaji huo ulikuwa ukifanyika kuanzia Desemba mpaka march na sasa unafanyika October mpaka Desemba pia uboreshwaji wa miundombinu ya mashuleni.

Kwa upande wa waalimu akiwepo Mwalimu wa darasa la awali  Neema Ngonyani Shule ya msingi Ruangwa  amesema miongoni mwa changamoto wanayokabiliana nayo walimu kwa wanafunzi wanaochelewa kuandikishwa shule ni kushindwa kuwafundisha katika mtiririko unaotakiwa huku  mwalimu wa darasa la kwanza Elizabeth Masue  akibainisha kuwa kitendo cha wanafunzi kuchelewa kuandikishwa shule kinafanya  walimu kuwa na mlundikano wa majukumu mengi.

“ile January ninapofungua shule ninakuwa na azimio la kazi kuanzia ile wiki tunayofungulia kama ni ya kwanza  au ya pili kwa hivyo ninavyofungua natakiwa kuwafundisha wale watoto sasa mwingine anakuja wa pili mwingine wa tatu  lazima atakuwa tofauti na yule aliekuja mwezi wa kwanza hivyo inanilazimu kutafuta muda wa ziada ili kumfundisha yule aliyechelewa kufika shule ili awezekuwa sawa na wengine vinginevyo nisipofanya hivyo nikitoa mazoezi au mitihani darasani hataweza kufanya vizuri kwa sababu vile vitu hajavisoma”amesema Mwl. Ngonyani.

“ile January ninapofungua shule ninakuwa na azimio la kazi kuanzia ile wiki tunayofungulia kama ni ya kwanza  au ya pili kwa hivyo ninavyofungua natakiwa kuwafundisha wale watoto sasa mwingine anakuja wa pili mwingine wa tatu  lazima atakuwa tofauti na yule aliekuja mwezi wa kwanza hivyo inanilazimu kutafuta muda wa ziada ili kumfundisha yule aliyechelewa kufika shule ili awezekuwa sawa na wengine vinginevyo nisipofanya hivyo nikitoa mazoezi au mitihani darasani hataweza kufanya vizuri kwa sababu vile vitu hajavisoma”amesema Mwl. Ngonyani.

Baadhi ya wazazi Wilaya ya Ruangwa wasiotaka kutaja majina yao wametaja sababu za kucheleweshwa kuripotishwa Kwa wanafunzi hadi kufika february hii ni ugumu wa Maisha hivyo kukosa baadhi ya mahitaji kama vifaa vya shule  huku Wazazi Wengi wakihamasika kupeleka watoto wao mashuleni kupitia hamasa na elimu inayotolewa na mkuu wa wilaya kupitia ziara yake ya kata kwa kata wilayani hapa.