Ruangwa FM

kuelekea miaka 59 ya muungano Lindi yazindua siku ya upandaji miti kimkoa

20 April 2023, 7:46 pm

Mkuu wa wilaya ya Kilwa akipanda mti wa matunda. picha :khadija omary.

Na loveness Daniel

Kuelekea maadhimisho ya sikukuu ya miaka 59  muungano wa Tanganyika na Zanzibar  ambayo hufanyika April 26 kila mwaka Mkoa wa Lindi umezindua siku ya upandaji miti kimkoa ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa hivi karibuni ambapo aliagiza sherehe hizo kwa mwaka 2023 zifanyike kwa ngazi za mikoa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika April 19 2023 katika shule ya Sekondari ya Wasichana Lindi Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi,  Mkuu wa Wilaya hiyo Shaibu Ndemanga ameagiza zoezi hilo la upandaji miti kuwa Endelevu katika taasisi zote serikali na watu binafsi na hasa uanzishaji wa bustani za miti ya matunda mashuleni.

sauti mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.

Christopha Ngubiagai ni mkuu wa wilaya ya Kilwa ameeleza moja ya changamoto inayoathiri misitu katika wilaya hiyo na maeneo jirani ni uanzishwaji wa mashamba mapya ya ufuta huku afisa muhifadhi mwandamizi wakala wa misitu Tanzania TFS Lukas Sabida akieleza namna TFS inavyoshirikiana na na wadau wengine katika kutunza na kuhifadhi misitu.

sauti DC kilwa na mhifadhi misitu TFS