Ruangwa FM
Ruangwa FM
9 June 2026, 13:17

Hali ya mimba za mapema wilaya ya ruangwa Bado imekua tishi wilaya ya ruangwa ikiwa January to march asilimia 16 huku awamu ya April ni 15 tofauti na takwimu kubwa hapo awali.
Akizungumza Jun 8 2026 katika kipindi Cha radio Jamii Ruangwafm katika kipindi Cha bodaboda mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wilaya ya Ruangwa Dr Fabiola Nyaki amesema kulingana na kiwango Cha serikali cha angalau asilimia 15 wilaya inajitahidi kutoa elimu dhini ya mimba za mapema kwani Zina madhara menginya kifya na kiakili.
Akizungumza mtendaji wa dawati la jinsia wanwake na watoto wilaya ya Ruangwa Sajenti Happy Lyatu amesema Mila kandamizi za kubebana kiujamaa zinakwamisha mapambano dhidi ya mimba za utotoni huku baadhi ya Sheria kuataja kua kikwanzo dhidi ya mapambano ya mimba za mapema.
Afsa ustawi Mwalimu Abdalah wilaya ya ruangwa amewataka wazazi kuwekeza katika mazungumzo na maadili huku akiwataka wazazi kuacha tabia ya kuendekeza ushauri wa uzazi wa mpango kwa watoto kwani kunachangia watoto kutohofia mimba za mapema na kuwa na maadili mabovu yanayopelekea ndoa za utotoni.
Baadhi ya wazazi katika kipindi hicho wamesema suala la baadhi ya wazazi kuwategemea watoto katika kipato ni chanzo Cha mimba za utotoni huku wengine wakiomba marekebisho ya Sheria ya ndoa ili kutokomeza mimba za utotoni.