Ruangwa FM

Umiliki wa ardhi kiholela chanzo cha kukosa haki kisheria

23 June 2026, 14:14

Afisa Maendeleo ya Ardhi wilayani Ruangwa, Isihaka Panja. Na mpigapicha wetu

Wananchi wengi Ruangwa wametajwa kununua maeneo kiholela jambo ambalo limesababisha migogoro ya ardhi na kuwakosesha haki za kisheria za umiliki wa ardhi.

Na Mwandishi wetu

Akizungumza 22 June Afisa Maendeleo ya Ardhi Isihaka Panja amesema migogoro mingi imefika ofisini hapo huku baadhi yao ni wananchi kuvamia maeneo ya kijamii, migogoro ya mipaka na kuingia katika maeneo ya hifadhi.

Sauti ya Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Isihaka Panja

Akizungumzia upatikanaji wa Ardhi Tanzania mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Levina Ado amesema ikiwa umegaiwa , umerithi,upewa,ama kununua Aridhi bila ya kufuata taratibu za aridhi utakua mkaaji Haramu wa Aridhi

Sauti ya Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Levina Ado

Nao viongozi wa serikali ya kijiji wamewataka wananchi kutoishia ofisi za vijiji pekee kwani maridhiano ya hati ya kijiji hayampi jamii uhalali kamili wa umiliki wa eneo husika.

Sauti ya viongozi wa serikali ya kijiji

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamezungumzia uelewa wao katika umiliki wa ardhi huku wakitaja kukosa haki kwani wengi huuziana kindugu.

Sauti za wananchi