Ruangwa FM
Ruangwa FM
14 September 2026, 12:02

Wanawake waomba elimu zaidi juu ya Umiliki Ardhi kisheria huku mfumo dume ukitajwa kua kikwazo
Na Omari Mdigo.
Ruangwa – Lindi.
Baadhi ya wanawake Mkoa wa Lindi wameeleza kuwa umiliki wa ardhi umewapa usalama wa mali na fursa za kiuchumi, huku wakitaka elimu zaidi kuhusu haki zao za kisheria.
Mayasa Joroa amesema changamoto si mila pekee, bali pia ukosefu wa uelewa kuhusu taratibu na haki za wanawake katika umiliki wa ardhi.
Takwimu zinaonesha Mkoa wa Lindi, asilimia 18 ya wanawake wenye miaka 15 na zaidi wanamiliki ardhi peke yao, ikilinganishwa na asilimia 22.7 ya wanaume.
Aidha, zaidi ya hati 7,300 za ardhi zimesajiliwa Lindi, huku wanawake wakiwa na hati 832 pekee za umiliki binafsi, sawa na asilimia 11.4.
Wadau wanasisitiza kuwa mwanamke ana haki ya kumiliki, kusajili, kutumia na kunufaika na ardhi bila kubaguliwa kwa misingi ya jinsia.
Ardhi si mali ya mwanaume pekee elimu, usajili na uelewa wa haki ni msingi wa kuongeza usalama wa umiliki kwa wanawake.