Radio Fadhila

DC Chaurembo: Aliyejirekodi na kusambaza video chafu achukuliwe hatua

29 May 2023, 10:14 AM

Nanyumbu

Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Mariam Chaurembo ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya ya Nanyumbu kumkamata na kumchukulia hatua kali za kisheria mwanamke aliyetambulika kwa jina la Zakia Yassini mzaliwa wa Maswera wilayani humo, umri wake ukikadriwa kuwa kati ya miaka 24, kwa shutuma za  kutenda kosa la kujirekodi na kusambaza picha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.
Chaurembo ametoa agizo hilo wakati akizungumza wilayani humo na kutoa wito kwa wananchi kuacha kuendelea kusambaza video hiyo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na atakayekaidi atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katika hatua nyingine,  Chaurembo amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo  Kutumia simu kwa Manufaa ya kujiletea  maendeleo na Sio matumizi yanayovunja maadili na mila za Kitanzania.