Radio Fadhila

Madiwani waridhia wawili kufukuzwa kazi Kwa uzembe wao

14 February 2023, 5:41 PM

Madiwani waridhia wawili kufukuzwa kazi

Na, Lilian martin

Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, Wilayani Masasi, Mkoani Mtwara kupitia Baraza la Madiwani kwa kauli moja wameridhia kuwafukuza kazi wauguzi wawili wanaofanya kazi katika Hospitali ya Mkomaindo, Wilayani Masasi

Wauguzi hao wanadaiwa kufanya uzembe wa kushindwa kumuhudumia Mama Mjamzito kwa wakati na kusababisha mama huyo kupoteza maisha kwa kukosa huduma kwa wakati.

Aidha, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Masasi, Dkt. Salumu Gembe, ametoa wito kwa watumishi wa afya katika Hospitali hiyo kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma na kuwahudumia wananchi kwa weledi.

Tukio hilo lilitokea mnamo mwishoni mwaka jana

Mama mjamzito huyo alifika Hospitalini hapo na baada ya kushindwa kupata huduma kwa wakati ilipelekea kupoteza maisha kabla hata ya kujifungua