Radio Fadhila

Wafanyabiashara Soko la Mkuti wilayani Masasi Mkoani Mtwara wofia ugonjwa wa mlipuko watoa ushauri.

17 January 2023, 9:15 AM

MASASI.

Baadhi ya Wafanyabiashara wanaofanya  biashara zao katika Soko la Mkuti  Halmashauri ya Mji wa Masasi, wameshauri eneo la kuifadhia taka kwa muda  lililopo katika Soko hilo  liboreshwe kwa kuwekwa miundominu rafiki ya kutunzia taka hizo au liondolewe kwa kutafuta sehemu rafiki kutokana na mahali panapotumika sasa hivi kuifadhia taka hizo kwa muda, kutokuwa rafiki na wakati wa mvua usababisha kero kubwa, kutokana na mlundikano wa taka hizo kwa kushindwa kuondolewa kwa wakati hali ambayo wameitaja inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

Wafanyabiashara hao wamekuja na ushauri huo baada yakuonekana suala la kuondolewa taka kwa wakati katika eneo hilo kuwa ni tatizo ambalo linajiludia mara kwa mara.

Wafanyabiashara hao wametoa ushauri huo wakati wakizungumza na mwandishi wetu alipotembelea eneo hilo na kushuhudia mlundikano wa taka ngumu na inzi wakiruka ruka katika eneo hilo.

Aidha katika atua nyingine Wafanyakazi wanaozoa taka katika maeneo mbalimbali ya masoko katika halmashauri ya mji wa masasi, wameomba serikali iwafikilie kwa kuwaongezea mshahara kutokana na mshahara wanaopoke hivi sasa kutokizi  mahitaji yao ya kawaida ya kutunza familia ikiwemo kuwasomesha watoto wao.

 

Wafanyakazi hao wametoa ombi hilo wakati mwandishi wetu alipotembelea katika maeneo ambayo wafanyakazi hao wanafanya shughuli zao.

Pamoja na hilo wafanyakazi hao wameeleza kukabiliwa na    changamoto mbalimbali hasa za vifaa vya kufanyia kazi   na kuomba wadau  waweze kuwasaidia

Miongoni mwa vifaa wanavyoviitaji ni pamoja na gloves, viziba mdomo na pua Yaani Barakoa, viatu vikubwa gambuti, matenga ya kuzolea taka  na nguo za kufanyia kazi,

Aidha itakumbukwa mkuu wa mkoa wa mtwara kanali Ahmed Abbas  hivi karibuni akiongoza kikao kazi cha mapitio ya tasimini ya elimu mkoani humo mbele ya wadau wa elimu     alisisitiza  kuweka kipaumbele  suala la usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo .