Radio Fadhila

warsha elekezi kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi

5 Novemba 2021, 3:57 mu

Asasi ya Kiraia ya @HakiElimu imeendesha warsha elekezi kwa baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara inayohusiana na uandaji wa bajeti yenye mlengo wa kijinsia ikiwemo kutambua usawa kati ya mtoto wa kike na wakiume.

Warsha hiyo elekezi ya siku mbili leo na kesho imefanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya wilaya Masasi ulioyopo mjini Masasi.

Lengo kuu la warsha hiyo ni kutambua mambo ya msingi yanayopaswa kuingizwa kwenye uandaji wa bajeti ngazi ya Halmashauri yanayomkabili binti wa kike katika sekta ya elimu na kumfanya kushindwa kusoma na kupata elimu ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa.