Radio Fadhila

MASASI: KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa uhuru Luteni, Josephine Mwambashi amekataa kuzindua mradi .

1 September 2021, 4:46 AM

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa uhuru Luteni, Josephine Mwambashi amekataa kuzindua mradi wa maji wa Chipole uliopo kijiji katika cha Chipole halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara. Hali hiyo imejitoleza leo katika mbio za mwenge ambapo mwenge wa uhuru upo wilaya Masasi kwa ajili mbio hizo.

Luteni Josephine Mwambashi amesema mradi huo ambao umegharimu sh. milioni 365 umebainika kuwa na kasoro huku taarifa ya mradi iliyotolewa na Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA halmashauri ya mji wa Masasi inaonyesha mradi umetumia shilingi milioni Mia Nne jambo ambalo siyo kweli.

Kasoro nyingine ya mradi huo ni udanganyifu uliofanyika kwenye ununuzi wa mabomba taarifa inasema yamenunuliwa mabomba 20 jambo ambalo siyo kweli yaliyonunuliwa ni mabomba 19.Amesema katika mradi huo kuna upotevu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 30 ambazo hazijulikani zilipo.

Kufuatia kasoro hizo zilizobainika kwenye mradi huo wa maji wa Chipole ,kiongizi huyo wa mwenge Luteni Josephine Mwambashi amezikabidhi nyaraka zote za mradi huo kwa mkuu wa wilaya ya Masasi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru ili kuanza mara moja kuchunguza mradi huo.

Mradi huo wa maji Chipole ulianza kujengwa mwaka May 2020 na kukamilika February 2021 na umeanza kufanya kazi huku ukiwa na kasoro hizo.