Radio Fadhila

CHAMA Cha Mapinduz Kimewazawadia Vyeti Maalumu

26 Agosti 2021, 5:16 mu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kimewazawadia vyeti maalumu vya kutambua mchango na juhudi wanazozifanya ndani ya Chama hicho ikiwemo kufanikisha upatikanaji wa ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani mwaka 2020

Wanachama hao ambao baadhi yao walikuwa katika kamati za kamapeni katika maeneo mbalimbali ya uchaguzi, Jimbo la Ndanda, Masasi na Lulindi ambapo kamati hizo zilifanya vizuri kabisa.

Miongoni mwa makada ambao wamefanikiwa kuwazawadiwa vyeti hivyo ni pamoja na Joseph Peneza ambaye yeye amepatiwa cheti na Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Masasi kwa kujitoa kwa moyo kukifadhali Chama hicho usiku na mchana na mchango wake huo amefanikisha ushindi wa CCM Masasi.

Aidha, kada mwingine ambaye pia amezawadiwa vyeti hivyo ni Asinani Murji ambaye yeye ndiye alikuwa kampeni meneja mkuu wa uchaguzi katika jimbo la Ndanda.

Licha ya majina hayo waliozawadiwa vyeti hivyo ni wanachama zaidi 20 pia na wao wamepatiwa vyeti na kwamba Chama hicho kinatambua mchango wa wanachama wake wote.

Mwwnyekiti wa CCM wilaya ya Masasi , Edward Mmavele amesema Chama kinatambua na kuthamini wanachama wake wote kwa mchango wao ndani ya Chama hicho hivyo kinaendelea kushirikana vema bila ya ubaguzi au makundi. Vyeti hivyo vilitolewa jana kwenye mkutano wa Halmashauri KUU CCM ya wilaya Masasi uliofanyika mjini Masasi wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani uchaguzi ya CCM.