Radio Fadhila

MAMCU wafanya mkutano mkuu wa 21 wa mwaka

21 Aprili 2021, 12:24 um

WAKULIMA wa Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Masasi-Mtwara( MAMCU) hii leo April 21 – 2021 wanafanya mkutano mkuu wa 21 wa mwaka wenye lengo la kuchagua viongozi wa bodi wa Chama hicho ikiwemo kusoma mapato na matumizi.  

Mkutano huo unafanyika mkoani Mtwara katika ukumbi wa chuo cha ualimu Mtwara.
  Chama kikuu Cha Mamcu kinaundwa na vyama vya msingi( Amcos) zipatazo 165 kutoka wilaya za Masasi , Mtwara na Nanyumbu.

story Rabia nandonde