Micheweni FM
Micheweni FM
28 February 2026, 9:27 am

Wananchi katika wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba, wametakiwa kuacha kujenga katika maeneo yasiyo rafiki kwao ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Na Mwiaba Kombo
Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Ali SalimMattar, ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kugharamia athari mabadiliko ya tabia nchi na maafa katika ukumbi wa Halmashauri ya Micheweni.
Amesisitiza washiriki kuyafikisha mafunzo hayo sehemu husika ili jamii iweze kupata uelewa zaidi kuhusu mabadiliko ya tabianchi na maafa.
Kwa upande wao, Afisa TEHAMA kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Yusouf Said Yusouf, pamoja na Mkuu wa Divisheni ya Mawasiliano na Tahadhari za Mapema, Omar Ali Mohd, wamesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wananchi juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi, kwani mara nyingi madhara yanapotokea wananchi ndio wahanga wakuu
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema wamejifunza mambo mengi ambayo awali hawakuyafahamu, na wameahidi kuyafikisha sehemu husika ili jamii iweze kunufaika.