Micheweni FM

Pemba wamshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa hospitali ya wilaya

2 September 2025, 10:33 am

Daktari dhamana hospital ya Vitongoji chake chake Fatma Ahmed Mohd akizungumza na waandishi wa habari walipofika hospitalini hapo picha na (Mwiaba Kombo)

Wananchi kisiwani Pemba wamemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuwapatiwa Hospitali ya Wilaya katika kijiji cha Vitongoji.

Na Mwiaba Kombo

Shukrani hizo zimetolewa na wananchi hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, katika ziara maalumu ya kutembelea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.

Mmoja wa wananchi hao, Rushda Khamis Kasim, amesema kuwa kupatikana kwa hospitali hiyo kumeondoa adha ya kutafuta huduma mbali katika hospitali nyingine.

sauti ya Rushda Khamis Kassim

Naye Khadija Ali Salum amesema hospitali hiyo inatoa huduma bora, dawa muhimu zinapatikana, na kuwepo kwake kumechangia kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Sauti ya Khadija Ali Salum

Kwa upande wake, Daktari Dhamana wa hospitali hiyo, Fatma Ahmed Mohd, amesema hivi sasa hospitali ina uwezo wa kuhudumia zaidi ya wagonjwa 400 kwa siku, jambo ambalo hapo awali lilikuwa changamoto kubwa.

Amesema pia kwa sasa hakuna changamoto kubwa zinazowakabili wagonjwa kwani huduma nyingi muhimu zinapatikana moja kwa moja katika hospitali hiyo, bila ya kulazimika kuwapeleka wagonjwa Hospitali ya Rufaa ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani.

sauti ya daktari dhamana hospitali ya vitongoji Fatma Ahmed Mohd