Micheweni FM
Micheweni FM
24 July 2025, 12:35 pm

Mkurugenzi wa halamashauri ya wilaya yaMicheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba amewataka wafanyakazi wa diko la Tumbe kuhakikisha wanasimamia iapasavyo usafi katika diko hilo ili kuweza kuindokana na maradhi ambayo yanaweza kujitokeza endapo soko hilo halitokuwa safi kwani mazingira machafu huvutia wadudu kama vile mbu, inzi na panya ambao husababisha magonjwa kama malaria, kipindupindu, homa ya matumbo, na magonjwa ya ngozi.
Na Mwiaba Kombo
KAMATI za uvuvi pamoja na madalali wa diko la Tumbe wametakiwa kusimamia suala la usafi katika soko hilo ili liweze kuwa katika haiba mzuri na ya kuvulitia
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Micheweni Hamad Khatib Saleh wakati alipokuwa akizungumza na kamati hizo huko katika diko la Tumbe
Nae muhasibu mapato kutoka halmashauri hiyo Suleiman Nassor Tumu amewataka viongozi hao kuacha suala la muhali kwenye utendaji wa kazi zao.
Kwa upande wao katibu wa kamati ya uvuvi Tumbe Omar Hamad Salum na Sharif Khamis Omar wamewataka watendaji wa halmashauri hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa maslahi mapana ya serikali pamoja na kamati za maendeleo Tumbe ,na kuendelea kufanya kazi kwa mashirikiana baina ya kamati hizo na watendaji wa halmashauri.
Kikao hicho kimewakutanisha kamati za uvuvi tumbe ,madalali wa diko la tumbe pamoja na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Micheweni