Micheweni FM
Micheweni FM
13 June 2025, 10:51 am

Chama cha wananchi CUF ni miongoni chama kikongwe cha kisiasa ambacho kwa upande wa Zanzibar kilikuwa ni chama kikuu cha Upinzani kuanzia mwaka 1995 mpaka mwaka 2000 ambapo kuliingia migogoro ndani ya chama hicho na kusababisha kupotea kwa wanachama wake walio wengi na hata kupoteza majimbo mengi upande wa Zanzibar kutokana na migogoro hiyo.
Na Essau. Kalukubila.
Mjumbe wa baraza kuu Taifa kupitia chama cha wananchi CUF Dauda Kasingwa amewataka wananchama wachama hicho na wapenzi kuendelea kukiunga mokono katika kipindi hiki kinapoelekea kushindana na vyama vingine vya siasa kwenye uchaguzi mkuu October mwaka huu.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini katika kampeni ya kukijenga chama hicho ambapo wamekuwa wakizunguka mikoa yote Zanzibar na Bara.
Amesema kila chama kinapoingia kwenye mchakato wa kupata viongozi wa ndani chama cha siasa hujitokeza makundi mbalimbali ambayo yanasababisha kuwapoteza wanachama wao ,hali ambayo inapelekea vyama vya siasa kupoteza wanachama wengi kutokana na makundi hayo.
Nae Rehema John Muhema ambae ni Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Lindi na Mjumbe wa baraza kuu Taifa amesema kuelekea uchaguzi mkuu October mwaka huu chama cha wananchi CUF kikiwa kinaunga mkono na kusisitiza kushiriki uchaguzi wakiwa na kauli mbiu ya ‘yes election’
Sambamba na hayo Bi Rehema amewasisitiza na kuwaomba wananchi kuwa na ushirikiano ili chama chao kiweze Kushida katika uchanguzi ili waweze kushika dola wakiwa na umoja na mshikamano.
Kwa upande wake Hamad Khatib Juma ambae pia ni mtia nia ya Ubunge wa jimbo la Micheweni amesema niwakati wa kukipa nafasi chama cha wananchi CUF ambapo chamahicho kimeanzishwa kwa misingi ya haki sawa kwa wananchi wote.