Wanahabari wa Radio Jamii Micheweni wanolewa maadili ya habari
16 December 2024, 4:57 pm
Wandishi wa habari na wafanya kazi wa Radio jamii Micheweni wakipatiwa mafunzo ya maadili ya habari na mkufunzi Hilali Alikisanda Ruhundwa kutoka Radio TADIO.
Waandishi wa habari wapewa elimu ya maadili ya uandishi wa habari katika kituo cha Radio Jamii Micheweni ambayo mafunzo hayo yamewajenga vyema katika utumiaji wa mitandao ya kijamii na kuzingatia misingi ya kihabari.
Na Essau Kalukubila.
Waandishi wa habari na watendaji wa kituo cha Radio Jamii Micheweni Pemba wametakiwa kuendelea kufuata misingi ya kiuandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao ili kuendelea kuaminika na jamii.
Kauli hiyo ameitoa mkufunzi Hilali Alexander Ruhundwa kutoka Radio TADIO katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ja kijamii kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hivyo wanapaswa kuendana na mabadiliko.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 nivyema radio ikaendelea na majukumu yake bili upendeleo wowote kaatika kipindi hiki.
Nae Meneja wa kituo cha Radi jamii Micheweni Ali Masoud Kombo ameomba tasisi hiyo ya Radio TADIO kwendelea kushirikiana nao kwa pamoja ilikuweza kuandika habari zenye tija.
Kwa upande wake Kuruthum Ramadhani mwandishi na mfanyakazi wa radio jamii micheweni amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja mda mwafaka kutokana na na dunia ilipohamia katika mitandao ya kijamii huku akiahidi kwendelea kutumia mitandao hiyo ili aweza kuifikia jamii kubwa.
Sauti ya mkufunzi Hilali Alikisanda Ruhundwa kutoka Radio TADIO