Wafanyakazi wa halmashauri watakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano
15 December 2024, 12:15 pm
Ushirikiano katika maeneo ya kazi ni jambo muhimu katika kufikia malengo husika na utekelezaji wa majukumu katika kuwasaidia wananchi
Na Kuruthum Ramadhan
Watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba watakiwa kufanya kazi kwa mashirikiano ili lengo la Serikali liweze kufikiwa .
Ameyasema hayo mkuu wa wilaya Micheweni Khatibu Juma Mjaja wakati alipokuwa na kikao na wafanya kazi wa ofisi ya halmashauri hiyo huko ofisini kwao Wingwi.
Amesema endapo wafanyakazi hao watafanya kazi kwa masharikiano mambo yatakwenda sawa kwani ofisi ya mkuu wa wilaya na halmsahauri wote lengo lao ni moja.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Micheweni Sheha Mpemba Faki amewataka watendaji wa halmashauri hiyo kumpa ushirikiano wa kutosha mkuu huyo wa wilaya ila adhma iweze kufikiwa .
Nae mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Hamad Mbwana Shehe pamoja na afisa utawala wa halmashauri hiyo ambae pia ni afisa uendeshaji Khamis Seif Ali wamesema watayafanyia kazi yale yote ambayo mkuu huyo wa wilaya ameyasema na pia wamemtaka mkuu huyo kuacha makundi katika utendaji wa kazi zake.
Mkuu wa wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja amefika kwa mara ya kwanza katika ofisi za halmashauri hiyo baada ya kupata uteuzi hivi karibuni wa kubadilishiwa kituo cha kazi ambapo kabla ya kuja Micheweni alikuwa mkuu wa wilaya ya Mkoani.