Micheweni FM

Tamwa yazitaka asasi za kiraia na tasisi za Serekali kushirikiana

15 December 2024, 12:00 pm

Wanawake ni kundi kubwa linalokabiliwa na umasikini lakini kupitia kilimo msitu kitaweza kuwakomboa kiuchumi.

Na Time Khamis Mwinyi

‎‎Chama cha wandishi wa habari wanawake Tazania Tamwa Zanzibar kisiwani Pemba wamezitaka asasi za kiraia na tasisi za Serekali kutowa ushirikiano katika kutekeleza mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi.

‎kauli hio imetolewa na Meneja wa Mradi wa ZANZADPT  Zoni ya Pemba  Ali Hamad wakati alipokuwa akitowa utambulisho wa mradi kwa asasi za kiraiya na tasisi za Serekali katika ofis za SHIJUWAZA  Chake Chake Pemba.

‎Amesema katika mradi huo wa

‎kukabiliana na mabadiliko ya Tabiya  nchi yamekuja kuwakomboa wanawake Katika nyanja mbali ikiweo kiuchumi na kuweza kupaza sauti katika kutetea haki zao.

‎Wakati huo huo Nairat Abdullah Ali Afisa Program kutoka

‎TAMWA_Zanzibar amesema Kila mmoja anajukumu la kuchukuwa hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabiayanchi hasa Kwa kutumza mazingira kwakupanda Miti Ili kukabiliana na mabadiliko hayo ambayo yamekuwepo Kwa kiasi kikubwa.

‎Nae Juma Bakari Alawi mratibu AZASPO Pemba ameipongeza  Tamwa Zanzibar kwa kushirikiana na washirika wa Mradi huo  kwa kuchukua jitihada za kuazisha mradi huu, utasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabiayanchi, kwani Kuna maeneo mengi yameanzaa kupotea  uhalisia wake hususan katika maeneo ya baharini.

‎Haji Nassor Mohd  kwa niamba ya wandishi wezake wameomba Jumuiya ya   Wandishi wa Habari Wanawake Tamwa Zanzibari kuwashirikisha watu wenye mahataji malum wakati wautekelezaji wa Mradi huo ili kuweza kukabiliana na Mabadiliko ya Tabiya ya nchi.

‎Amesema ipo haja ya kutolewa elimu kwa mwalim ToT kwani wamesema hawakuwashirikisha watu mwenye mahitaji malum kutokana hali zao jambo ambalo litapelekeya kuwakosesha haki ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabiaya ya nchi.

‎Jumuiya ya Uhifadhi wa Msitu Pemba CFP  inautambulisha mradi wa ZANZADPT kwa wadau kisiwani Pemba na kuelezwa kuwa  asilimia 80 wanufaika ni wanawake.