Wanawake watakiwa kuchangamkia fursa michezoni
25 November 2024, 9:59 am
Michezo ni moja kati ya fursa ambazo zinaifanya jamii kujikomboa na hali ngumu ya kimaisha ambazo zimekuwa zikitukabili katika jamii zetu
Na Mwiaba Kombo
Nimatumaini yangu hujambo mpenzi wa 97.4 Micheweni Fm nikukaribishe katika Makala maalum ambapo kwa siku ya leo tutazungumzia fursa ambazo wanaweza kuzipata wanawake endeka watashiriki michezo Mkoa wa kaskazini Pemba ambapo Makala hii inaletwa kwako na Mwiaba Kombo Hamad, kwa ushirikiano wa Chama Cha Waandishi Wa Habari Wanawake, Tanzania, Zanzibar (TAMWA Zanzibar),kupitia mradi wa Michezo kwa Maendeleo unaotekelezwa chini ya ufadhili shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ) nikusihi tuwe pamoja mwanzo hadi mwisho wa Makala hii .
Fursa ni mtu anavyoweza kutazama jambo au kitu na kubuni manufaa yake au jamii kutokana na jambo au kitu Fulani anachokitazama ,anachokiona au anachokifikiria.