Taasisi za Serikali na binafsi zatakiwa kujenga majengo ya kudumu Chamanangwe
19 October 2024, 3:43 pm
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar na Mipango mikakati mbali mbali inaendelea kuwawekea mazingira wezeshi wananchi ya kuekeza katika kilimo chenye tija kwa chakula na biashara ambacho kitakuza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Na Mwiaba Kombo.
WAZIRI wa Kilimo, Umwagiliaji , Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema uwepo wa taasisi za Serikali na binafsi kutoka Zanzibar na Tanzania Bara imekuwa ni chachu ya mafanikio ya maonyesho ya siku ya chakula yaliyofanyika katika kiwanja cha Chamanangwe Kisiwani Pemba.
Akizungumza na wandishi wa Habari wakati wa kuahirisha maonyesho hayo, Mhe Shamata amesema matumizi sahihi ya taaluma iliyotolewa wakati wa maonyesho hayo imeibua hisia za wakulima na wafugaji ya kuendesha shughuli zao kitaalamu.
Mhe Shamata amesema eneo la Chamanangwe litakuwa kituo cha kutoa elimu na taaluma za kilimo na ufugaji kwa kipindi chote na kuwataka wananchi kuendelea kulitumia kwa ajili ya kujifunza taaluma mbali mbali..
Aidha amezita taasisi zilizokabidhiwa viwanja katika eneo hilo kuhakikisha wanaweka makaazi ya kudumu ili iwe rahisi kwa wananchi kupata taaluma.
Mhe Shamata ametoa wito kwa taasisi mbali mbali kuhakiksha wanajenga majengo ya kudumu katika maeneo hayo ili kupunguza gharama ya kila mwaka .
Mapema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasilia na Mifugo dkt Omar Ali Amir amesema maonyesho hayo yemeleta tija kwa wananchi wa bara na visiwani kwani wananchi waliowengi wamefika na kujifunza vitu mbali mbali .