JAMII
Micheweni FM

7000 watoroka Skuli Wilaya ya Micheweni

1 October 2021, 9:12 am

DC MICHEWENI AZUNGUMZA NA WAZEE WA SHUMBA MJINI

Na Ali Kombo

PEMBA

Zaidi ya Wanafunzi 7000 wilaya ya Micheweni hawaendi skuli na kuifanya wilaya hiyo ikawa inaongoza kwa wanafunzi walio watoro licha ya kuonekana ni ya mwanzo kitaifa kwa wanafunzi waliofaulu

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Mgeni Khatibu Yahya wakatialipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha shumba ya mjini katika siku ya habari duniani na kuwataka wazee na walezi kushirikiana ili kuondoa tatizo hilo

Amesema wanafunzi watakaposoma na kufaulu vizuri tunaweza kupata wahandisi pamoja na wataalamu ambayo wataifanya micheweni kuwa kitovu cha maendeo

Hata hivyo kaimu mratbu mamlaka ya usafir Baharini Pemba Fadhili Maulid Fadhili amesema wameambua kusajili vyombo vya baharili ili kutambulikana wakati watakapopotea

Naye Muhandisi Farida shaabani amesema wameamua kuhamasisha wanawake kujiunga na maswali ya baharini ili kuendana sambamba na uchumi wa buluu

Kwaupande Bidawa Bakari Hamadi wa kiji cha shumba ya mjini amesema wanaomba kujengewa na mnara wa kuongozea vyombo ili watakapopea baharini waweze kuongoza na huku Mbasho Rashid Hoseni amesema chuo zinazofundisha ubaharia wapungeze ada ili wajiunge na masomo