PEGAO, TAMWA ZNZ, ZAFELA zaahidi kuendelea kutetea ushiriki wa wanawake katika uongozi.
1 October 2021, 7:47 am
Na Gaspary Charles.
Jumuia ya utetezi wa kijinsia na mazingira pemba( Pegao) imesema itaendelea kushirikiana na wanawake wote wanaotaka kugombea nafasi za uongozi katika kutatua changamoto zinazowarudisha nyuma kufikia lengo hilo katika nyanja mbali mbali za siasa, democrasia na uchumi
Ameyasema hayo Mkurugenzi wa Jumuia hiyo Pemba Hafidh Abdi Said katika mkutano maalum wa uhamasishaji jamii juu ya wanawake kudai haki za uongozi uliofanyika kinyikani mchangamdogo mkoa wa kaskazini pemba.
Amesema endapo wanawake watakuwa na dhamira ya kugombea nafasi za uongozi na kukutana na changamoto jumyia hiyo itasaidia kulitimiza lengo hilo ili fursa hiyo kwa muda stahiki.
Wakizungumza katika mkutano huo wahamasishaji jamii kutoka pegao Akiwemo Rukia Ibrahim, amewataka wanawake hao waliohudhuria katika mkutano huo kuwa mabalozi kwa wanawake wengine katika jamii juu ya kudai haki zao za uongozi katika nyanja zote.
Nao baadhi ya wanawake wa shehia ya kinyikani wameiomba pegao kuendela kuwahamisha kupata uzoefu wa kuondoa woga wa kudai haki zao za kuwa viongozi ili wajikomboe katika maendeleo pamoja na kuwapatia elimu kuhusu uongozi pamoja na kuwajengea uwezo juu ya suala hilo.
Aidha wameeleza kuwa changamoto kubwa zinazowakabili wanawake hao ni kukosa kujiamini wanapodhamiria kugombea kutokana na kukosa uzoefu wa kuzngumza na kudai haki zao mbele ya makundi ya watu majukumu mengi ya familia wanayoachiwa na wanaume.
Jumuia ya pegao inatekeleza mradi wa uhamasishaji jamii juu ya wanawake kudai nafasi za uongozi kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar pamoja na Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Zafela.