Viongozi wapya serikali za mitaa wapewa semina elekezi kata ya Oloirien Ngorongoro
20 December 2024, 8:49 am
Katika kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo viongozi walioshinda uchaguzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa iliyopita viongozi hao wamekutana pamoja kujengewa uwezo wa namna ya kutekeleza majukumu yao.
Na Saitoti Saringe
Akizungumza na wenyeviti hao pamoja na serikali za vijiji Disemba 19.2024. Mh. Killel Shengena Diwani wa kata hiyo amewashukuru viongozi waliomaliza muda wao kwa ushirikiano na kazi kubwa walioufanya kwa kipindi cha uongozi wao.
Aidha viongozi hao wamefanya tathmini ya pamoja juu ya Maendeleo ya kata kwa kuchambua Miradi mbalimbali ya Maendeleo zikiwemo Elimu, Afya,Miundombinu ya barabara,Kilimo, ufugaji na hali ya Maendeleo ya wananchi binafsi ili kubaini changamoto za wananchi sambamba na kuweka, Dira ya utekelezaji na uboreshaji kwa Mwenyeviti walioingia madarakani.
Hata hivyo viongozi hao wapya wa serikali za mitaa katika kata hiyo wameishukuru wananchi, serikali pamoja na Diwani wa kata hiyo na kuahidi uwajibikaji na uzalendo ili kutimiza lengo la serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
kikao hicho kilihudhuriwa na baadhi ya wananchi, Viongozi wa serikali na viongozi wa chama Chama Cha Mapinduzi Ngorongoro na kupongeza kata na viongozi kwa kazi nzuri ya kudumisha Umoja na mshikamano kwa viongozi na wananchi ili kuleta Maendeleo ya pamoja.