Balozi Msumbiji akoshwa na banda la Ngorongoro sabasaba
8 July 2024, 11:10 pm
Maonesho ya biashara yanayojulikana kama sabasaba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya biashara miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya biashara ya kimataifa Dar es Salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere.
Na mwandishi wetu.
Balozi wa Tanzania Nchini Msumbiji CGP (Mstaafu). Phaustine M.Kasike leo 09 Julai 2024 ametembelea banda la wizara ya maliasili na utalii kwenye maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara sabasaba Dar es Salaam na kujionea namna ambavyo hifadhi ya Ngorongoro inaonyesha vivutio vya utalii mubashara kutoka Ngorongoro.
Balozi Kasike ni miongoni mwa maelefu ya wananchi waliotembelea banda hilo na kupongeza ubunifu uliofanywa na wizara hiyo kupitia mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kutangaza vivutio vya utalii kwa kuwaonesha wananchi mubashara matukio yanayotokea hifadhini hali inayoongeza hamasa ya wananchi wanaoendelea kutembelea banda hilo.
Programu ya kuonesha matukio ya utalii mubashara kutokea Ngorongoro itaendelea katika banda la wizara ya maliasili na utalii hadi tamati ya maonesho hayo tarehe 13 Julai, 2024.