Loliondo FM

Migogoro chanzo chama cha soka Ngorongoro kusimamishwa

13 April 2025, 11:01 pm

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Arusha (ARFA) Ndg, Zakayo Mjema ,picha na mpiga picha.

Katiba ya ARFA inaeleza kwamba mtu yeyote asipofanya kazi ya mpira ndani ya mwaka mmoja na hata wale ambao hawata chezesha Ligi za U-20 watakuwa wamepoteza sifa za kuwa wanachama.

Na Edward Shao.

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Ngorongoro akiri kusimamishwa uanachama wa mpira wa miguu mkoa wa Arusha.

Akizungumza hii leo Aprili 13,2025 na Loliondo fm bw Batanisha Namjogo mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Ngorongoro (NGODIFA) amesema ni sahihi kwa wao kusimamishwa uanachama wa chama hicho kwani wemeshindwa kutekeleza majukumu yao ya soka kama vile,kuanzisha ligi ya wilaya,kuanzisha mashindano mbalimbali ya wilaya na kutoa taarifa za chama icho mkoani.

Sauti ya Batanisha Namjogo

Ameeleza chanzo kikubwa cha wao kushindwa kutimiza majukumu yao na kupelekea wao kusimamishwa uanachama ni migogoro ya kiuongozi ndani ya chama icho na amekuwa akitimiza majukumu ya kisoka peke yake tangu uchaguzi wa chama ulipofanyika mwaka 2023 na yeye kuwa mwenyekiti ambapo baadhi ya wajumbe hawakutaka yeye awe kiongozi, hivyo hapati ushirikiano kutoka kwa makamu mwenyekiti na katibu wa chama.

Sauti ya Batanisha Namjogo

Hata hivyo Batanisha amesema atachukua hatua ya kuita viongozi wa jumuiya ya michezo tarafa ya Sale na Loliondo aliyoiunda kuendesha maswala ya kimichezo kujadili nini wafanye kuhusu kusimamishwa uanachama kabla ya kumshirikisha mlezi wa NGODIFA ambaye ni katibu tawala wa wilaya.

Sauti ya Batanisha Namjogo

Akitangaza uamuzi wa kusimamishwa uanachama wa chama cha soka wilaya ya Ngorongoro (NGODIFA)mwenyekiti wa ARFA ndg Zakayo Mjema Aprili 12,2025 katika mkutano mkuu wa chama hicho mkoa wa Arusha kilichofanyika wilayani Karatu amesema wilaya ya Ngorongoro amishindwa kufanya shughuli zozote za kisoka ndani ya miaka 3.

Sauti ya Zakayo Mjema