Mahakama yapiga stop vijiji kufutwa Ngorongoro
22 August 2024, 10:33 pm
Baada ya kuwepo kwa taarifa za kufutwa kwa baadhi ya vijiji wilayani Ngorongoro kumekuwepo wadau mbalimbali wa kutetea haki za wanangorongoro kuhakikisha wanapata haki na huduma zao za msingi kama ilivyo kwa wananchi wengine hapa nchini.
Na mwandishi wetu.
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imesimamisha utekelezaji wa amri iliyokuwa imetolewa na serikali kupitia tangazo la serikali namba 673 ya 2024 la kufuta vijiji, kata na vitongoji pamoja na kusitisha tangazo la kuwataka wananchi kuhama katika wilaya ya Ngorongoro.
Umuamuzi huo umetolewa leo Agosti 22, 2024 mbele ya Jaji Mwenda wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha katika kesi namba 59630 ya mwaka 2024 kufuatia maombi yaliyopelekwa mahakamani na mpeleka maombi Isaya Ole Posi ya kuiomba ipime na kutazama kama amri ile ilikuwa halali au la hasha au kama ilitolewa na mtu mwenye mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.
Wakili wa kujitegemea Peter Njau akimewakilisha mteja wake Isaya Ole Posi amesema mteja wake alikuwa mwathirika wa kuondolewa katika eneo hilo jambo ambalo aliamua kwenda mahakamani kupinga kitendo hicho.