Loliondo FM

CHADEMA: Tatizo la Ngorongoro haliwezi kumalizwa na mitutu ya bunduki

22 August 2024, 3:20 pm

Mwenyekiti wa CHADEMA mh Freeman Mbowe picha na mpiga picha

Hakuna tamko lolote rasmi kutoka serikalini kuhusu maandamano ya wananchi wanaoishi tarafa ya Ngorongoro kuhusu kero mbalimbali zinazowakabili.

Na mwandishi wetu.

Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kupitia mwenyekiti wa chama hicho mh Freeman Mbowe wametoa tamko na msimamo wao kuhusu yanoendelea Ngorongoro.

Ameyasema hayo hii leo Agosti 22,2024 wakati ikizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Tunaitaka serikali irejeshe haraka huduma zote za kijamii kwa jamii yote ya Ngorongoro, mamlaka za uchaguzi zirejeshe haraka haki ya wananchi wote wa Ngorongoro kushiriki michakato yote ya kuwapata viongozi, kuchagua na kuchaguliwa na kuwapata viongozi wao, hata kama kuna migogoro, mgogoro hauwezi kuisha kwa kuwanyima watu haki za msingi”

“Tunamtaka Rais tena kama mfariji mkuu atumie mamlaka yake kurejesha haki za kiraia kwa wananchi wa Ngorongoro, hakuna sababu yoyote inayoweza kuelezeka kuwanyima wananchi hawa haki zao za kiraia, katiba ya nchi yetu inatoa haki ya kuishi, kusikilizwa, haki ya kutokutwezwa”

“Bila kujali nani amesimama wapi, tatizo la Ngorongoro haliwezi kumalizwa kwa mitutu ya bunduki ndio msimamo wa Chadema,mtamwaga damu zisizo na hatia mtaumiza taifa hili mtachagua machafuko haya yatasambaa nchi nzima”. mwenyekiti wa chadema.

Sauti ya Mbowe