Loliondo FM

NCAA: Shughuli za utalii zinaendelea Ngorongoro pamoja na uwepo wa maandamano

18 August 2024, 8:59 pm

Baadhi ya wananchi waishio tarafa ya Ngorongoro wakiandamana (picha na mpiga picha).

Idadi kubwa ya wananchi wanaoishi katika tarafa ya Ngorongoro wameandamana hii leo Agosti 18,2024 wakishinikiza serikali iwasikilize na kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili.

Na mwandishi wetu.

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kuwa shughuli za utalii bado zinaendelea katika hifadhi hiyo licha ya uwepo wa maandamano.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na kaimu meneja kitengo cha uhusiano kwa umma bw,Hamis Dambaya imeeleza kuwa shughuli za utalii zinaendelea vizuri pomoja na uwepo wa wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo kuandamana leo tarehe 18.08.2024.

Imeongeza kuwa watalii kutoka ndani na nje ya nchi wameendelea na safari zao za kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya hifadhi na serikali unaendelea kuwahakikishia usalama wao.

Hata hivyo taarifa hiyo imesema maandamano yaliyoripotiwa kupitia baadhi mitandao ya kijamii yanaidhihirishia dunia na jumuiya za kimataifa, vyombo vya habari na asasi za kimataifa kwamba, ndani ya hifadhi hiyo hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu na unyanyasaji wa wananchi.

NCAA imeongeza kuwa inawahakikishia watalii wote waliopanga safari za kwenda Ngorongoro kuwa serikali itaendelea kusimamia usalama wao wakati wote watakapokuwa ndani ya hifadhi hiyo.

Taarifa kwa umma kutoka NCAA.