Loliondo FM

PALISEP yazindua mradi, kuwafikia wananchi 15,000 Ngorongoro

18 July 2024, 10:17 am

Mkurugenzi wa sShirika la Lalisep Be Robert Kamakia akifafanua jambo mbele ya viongozi mbalimbali wa halmashauri ikiwemo Mkuu wa Wilaya Kanali Wilson Sakulo kuhusu mradi wa uhifadhi walioutambulisha.(Picha na mpiga picha wetu).

Mashirika mengi yasiyo ya kiserikali wilayani Ngorongoro yamekuwa yakitekeleza miradi mingi yenye manufaa kwa jamii za kifugaji ikiwepo maswala ya uhifadhi, mabadiliko ya tabia ya nchi na mingine mingi.

Na Edward Shao.

Shirika lisilo la kiserikali PALISEP limezindua mradi wa uhifadhi kuwafikia jamii za kifugaji na jamii asilia katika tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro.

Akizungumza Julai 17, 2024 kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilvaya ya Ngorongoro mkurugenzi wa shirika la Palisep Bw Robert Kamakia amesema leo anayo furaha kubwa kwa kufanikisha uzinduzi na utambulisho wa mradi wa uhifadhi ambao watakao utekeleza katika wilaya ya Ngorongoro tarafa ya Loliondo kwa kushirikiana na viongozi pamoja na wananchi.

Amesema kuwa wanalenga kuwafikia jamii za kifugaji na jamii za asilia ambapo wataufanya katika msitu wa Sarian uliopo katika Kijiji cha Olorien kuhakikisha kuwa msitu huo unatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae.

Bw Robert ameongeza kuwa wanalenga kuwafikia wananchi wa asili 15,000 kwa kupata maji safi na salama na kuwafikia mifugo 50,000 na kuwasaidi kina mama,vijana na makundi maalum kufanya shughuli za kiuchumi kama vile uzalishaji wa asali kwa kuwanunulia mizinga ya nyuki pamoja na kuwafundisha kuhusu maswala ya tabia ya nchi na uhifadhi kwa ujumla.

Sauti ya bwn Robert

Naye Bw Julias Parimayo afisa mtendaji kijiji cha Olorien amelishukuru shirika la Palisep kwa mradi huo kufanyika katika kijiji chake na kuomba wananchi wake kutoa ushirikiano kwa shirika hilo huku akitaja baadhi ya njia zinazoaribu vyanzo vya maji katika msitu wa Sarian ni pamoja nakinamama kukata kuni na mifugo kupita karibu na vyanzo vya maji.

Sauti ya Mtendaji

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Oloren Bw Parimaari amesema walikuwa wanahuitaji wa kupata msaada wa kufensi chanzo cha maji kwenye msitu wa Sarien na kufensi kiasili kwa kutumia magogo hivyo mradi huo wa uhifadhi unaolenga kuifadhi chanzo hicho kutoka shirika la Palisep ni muhimu kwani wananchi wa kijiji cha Olorien wanahuitaji mkubwa.

Sauti ya mwenyekiti