Loliondo FM

Wananchi Ngorongoro hawatumii maji kuhofia laana

2 July 2024, 6:44 am

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo kulia akizungumza jambo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Bw. Murtallah Sadiki (Picha na Zacharia James.)

Elimu bado inahitajika kwa wananchi katika jamii za kifugaji kuhusu matumizi safi ya maji na utunzaji wa mazingira, kulinda vyanzo vya maji na kulinda miundombinu ya maji katika matumizi yao ya kila siku ikiwemo wakati wa unyweshaji wa mifugo maji.

Na Edward Shao.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo amewataka madiwani na wenyeviti wa vijiji kuhamasisha wananchi kujiunga na vyombo vya utoaji wa huduma ya maji.

Ameyasema hayo hii leo Julai Mosi 2024 katika mkutano mkuu wa nusu mwaka wa vyombo vya utaoji wa huduma ya maji vijijini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambapo Kanali Sakulo amewataka waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwenda kuhamasisha wananchi watumiaji wa maji waongezeke ili kuongeza mapato ya vyombo vya utoaji wa huduma ya maji ngazi ya jamii CBWSOs kwani serikali inatumia pesa nyingi katika miradi hiyo ya maji na hata wafadhili wengi kujitokeza ni kwa sababu ya Rais Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya

Akizungumzia malengo ya mkutano huo, afisa maendeleo ya jamii kutoka RUWASA Bwn Enock Mwakanyamale amesema mkutano huu ni mkutano wa nusu mwaka wa vyombo vya utoaji wa huduma ya maji ngazi ya jamii mahsusi kwa ajili ya kukutanisha vyombo hivyo CBWSOs pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya maji na kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira vijijini na kuongeza ubora, ufanisi na utendaji kazi wa vyombo hivyo ndani ya jamii ili wananchi wanaoishi vijijini wapate huduma ya maji wakati wote.

Sauti ya Enock

Kwa upande wake diwani kata ya Sale Mh. Hamza J Masedo amesema elimu bado inahitajika kwa wananchi kutumia maji yanayosimamiwa na CBWSOs kwani wengi wao wanaogopa kulaaniwa na kufa kutoka kwa wanamije ambao ni viongozi wa kimila.

Sauti ya Diwani

Mkutano huu Umefanyika chini ya Wakala wa Usambazaji wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo,mkugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro bw Muratallah Sadiki,katibu tawala,makamu mwenyekiti wa ccm wilaya,viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa usimamizi wa vyombo vya utoaji wa huduma ya maji ngazi ya jamii [CBWSOs.