Loliondo FM

Jamii ya Maasai kuongozwa na viongozi wa kimila wanawake

19 June 2024, 4:44 pm

Viongozi wa kimila Ingagwanak waliosimikwa kwenye picha ya pamoja na mkurugenzi wa shirika la Memutie bi Rose Njilo wakwanza kushoto na wapili kushoto ni mwenyekiti wa UWT bi Fatuma Ngorisa,(picha na Edward Shao).

Ni mara chache kushuhudia viongozi wa kimila wanawake wameaminiwa na kupewa nafasi katika kuongoza jamii, lakini shirika la Memutie limefanikiwa kuielimisha jamii ya kimaasai na kukubali kupata viongozi wa kimila wanawake maarufu Ingaigwanak na kuwasimika rasmi tayari kuanza majukumu yao.

Na Edward Shao.

Shirika la Memutie Women Organization limewasimika viongozi wa kimila wanawake Ingaigwanak wilaya Ngorongoro.

Sherehe hiyo kubwa ya usimikaji wa viongozi hao wakimila imefanyika kata ya Maalon Juni 18,2024 ikiudhuriwa na viongozi wa kiserikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Akizungumza katika sherehe hiyo na tukio la kihistoria mgeni rasmi bwn Hamza H Hamza katibu tawala wilaya ya Ngorongoro kwa niaba ya mkuu wa wilaya amesema shirika la Memutie ni shirika la kuigwa kwa mambo wanayoyafanya na wao serikali wapo tayari kufanya kazi na wadau wote wa maendeleo.

Ameongeza kuwa tukio lilofanyika ni tukio la kihistoria kwani katika maisha yake akuwai kushuudia viongozi wa kimila wanawake wanaaminiwa katika vyombo mbalimbali vya kimaamuzi hasa katika taratibu za kimila kwani jamii nyingi azitambui nafasi ya mwanamke katika kufanya maamuzi ikiwepo jamii ya kimasai.

Sauti ya katibu tawala

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la Memutie Bi Rose Njilo Amesema tukio hili la kuwasimika ingaigwanak sita limeusisha kata sita wilayani hapa ambazo ni kata za Maalon,Malambo,Piyaya, Arash, Olorien na Engusero sambu huku akitaja lengo kuu kuhakikisha wanawake kushiriki katika vyombo vya kutoa maamuzi ngazi ya kijamii na kuleta mabadiliko chanya katika kupambana na maswala ya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Sauti ya Rose Njilo

Miongoni mwa Ingaigwanak waliosimikwa bi Naisho Saipu amesema shirika la Memutie ndilo lilowapatia elimu kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi katika jamii na wao kabla ya kupata hiyo elimu walikuwa wanakumbuna na vitendo vya kikatili ikiwepo ukeketaji pia ameomba serikali kuwaunga mkono viongozi hao wa kimila katika mapambano ya kutokomeza mfumo dume katika jamii na kutokupokea rushwa.

Sauti ya Naisho

Naye bwn Lengumo Parimiria ambaye ni laigwanan wa mila kutoka kata ya Engusero sambu amesema wapo tayari kushirikiana na Ingaigwanak hao waliosimikwa na kuwapa ushirikiano huku akisema watafanya kikao cha Malaigwan na Ingaigwanak waliosimikwa hii leo.

Sauti ya Lengumo

Sherehe hii kubwa na yakihistoria imeudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo mwakikishi kutoka mtandao wa wanawake watetezi wa haki za wanawake Tanzania pamoja, mwakikishi kutoka mfuko wa ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust), viongozi wa chama cha mapinduzi ccm, madiwani viti maalum na wananchi wa kawaida.