Aliyefichwa kwa miaka 13 kisa ulemavu aibuliwa Ngorongoro
31 May 2024, 2:36 pm
Jamii za kifugaji zinazo patikana katika wilaya ya Ngorongoro baadhi yao wanaamini mtu mwenye ulemavu kwenye familia ni laana au mkosi hivyo wengi wao uwaficha wasionekane katika jamii.
Na Edward Shao.
Shirika la Ngolac [Ngorongoro legal aid center] limefanikiwa kumuibua mtoto Elewa Mgonde [13]mwenye ulemavu wa macho mkazi wa kijiji cha Oldonyo sambu wilayani Ngorongoro na kumsaidia kumtafutia shule kwaajili ya kuanza masomo.
Akizungumza ofini kwake Mei 28,2024 katika hafla yakumpokea mtoto huyo bwn Moses Mereto Molell mratibu wa dawati la watu wenye ulemavu Ngorongoro ameishukuru redio Loliondo fm kwa jitihada za kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwaibua watu wenye ulemavu kupitia kampeni maalum inayoitwa “MSHIKE MKONO MTU MWENYE ULEMAVU” huku akiendelea kuikumbusha jamii kuwa ulemavu siyo kulemaa na siyo mwisho wa juhudi za kujiletea maendeleo.
Kwa upande wake mwl Ronald Mwende afisa elimu maalum wilaya ya Ngorongoro amesema wanahusika na kunatoa elimu kwa wanafunzi wenye uitaji maalum kwa kushirikiana na shirika la Ngolac katika kuwabaini watoto hao kwenye kaya zao pamoja na kuwapa huduma ya elimu na hadi sasa wamefanikiwa kuwabaini na kuwapitia huduma za kielimu watoto wanne huku akisema wamekwisha wabaini watoto wengine wilayani hapa na wanaendelea kuwatafutia shule kwaajili ya kupata huduma ya elimu.
Pia amebainisha kuwa wamekuwa wakitoa vifaa saidizi kwa watoto hao wenye uitaji maalum kama vile viti mwendo,fimbo nyeupe na vitabu vya maandishi makubwa.
Pamoja na hayo mwl Ronald ameongeza kuwa kwasasa wapo wanafunzi wenye uitaji maalum 259 kwenye halmshauri ya Ngorongoro wanauitaji wa vifaa saidizi ikiwemo wanafunzi 11 wa viti mwendo,wasioona 05 wakiitaji mashine za kuandikia huku akitaja changamoto kubwa ni ukosefu wa waalimu mwenye fani maalum ya kuwafundisha wanafunzi hao.
Licha ya mwanafunzi Elewa Mgonde aliyeibuliwa na shirika la Ngolac na kufanikiwa kumtafutia shule wilayani Longido bado baba wa binti huyo bwn Linus Mgonde amekuwa kikwazo kukubali kutoa ruhusa kwa mtoto huyo kwenda shule.