Aliyedaiwa kutumia milioni 400 kulala hotelini Ngorongoro akabidhi ofisi
11 May 2024, 12:24 pm
Baada ya kuhudumu kwa muda mfupi kwenye nafasi ya kamishina wa hifadhi,mamlaka ya Ngorongoro NCAA ndg Richard Kiiza na kuondolewa na rais Mh,Dr Samia Suluhu Hassan Machi 15,2024 hatimaye Mei 06 2024 rais amemteua Dr Elirehema Doriye kushika nafasi hiyo.
Na Edward Shao.
Kamishina mpya wa hifadhi, mamlaka ya eneo la Ngorongoro NCAA Dr Elirehema Doriye Mei 11 2024 amewasili makao makuu ya NCAA Karatu Arusha.
Dr Elirehema aliyeteuliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ameripoti makao makuu hayo huku akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa kamishina wa NCAA ndg Richard Kiiza tayari kuanza majukumu yake mapya.
Doriye aliwahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la bima la taifa (NIC).
Unaweza kusoma habari hii: Kamishna wa uhifadhi atumia milioni 400 kulala hotelini Ngorongoro
Ikumbukwe hivi karibuni diwani wa kata ya Alaitole mh James Moringe alimtuhumu ndg Kiiza kwa matumizi mabaya ya fedha za mamlaka hiyo ikiwepo kulala hoteli ya gharama kubwa.