Matukio ya mvua Ngorongoro mmoja afariki
22 January 2024, 1:29 pm
Katika Matukio makubwa ya wiki wilayani hapa yametawaliwa kwa kiasi kikubwa ni athari mbalimbali ambazo zimesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi ikiwemo mtu mmoja kupoteza Maisha baada ya kusombwa na maji.
Na Edward Shao,
Mvua zinazoendelea kunyesha hapa wilayani zimesababishwa mathara mbalimbali ikiwemo ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mborroekinyu Olormambuli Likay mkazi wa kijiji cha Pinyinyi kata ya Pinyinyi amefariki dunia baada ya kusombwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.
Mwenyekiti wa kijiji icho bwn Joshua Lekipa Laizer akithibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema lilitokea Januari 16,2024 na hili likiwa tukio la pili kwa kipindi cha wiki mbili katika Kijiji cha Pinyinyi kwani Januari mosi mwaka huu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Bwn Nassoro Shemzigwa alitoa taarifa ya kufariki dunia kwa afisa muuguzi msadizi zahati ya Pinyinyi ndg King’onde Sululu baada ya kusombwa na maji.
Wakati huo huo lori la mchanga likisombwa na maji siku ya Januari 19,2024 wakati likijaribu kuvuka daraja la Kapongoni barabara ya Wasso-Loliondo,huku kukiwa hakuna majeruhi wala vifo vilivyobainika kutokea kutoka na tukio hilo.
Katika mathara mengine yaliyotokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Ngorongoro ni pamoja na ukingo wa barabara ya Wasso-Sale eneo la mlima mdito ukiporomoka na kuziba sehemu ya barabara hiyo na kusababisha kero kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Mamlaka ya hali ya hewa hapa nchini TMA walitoa taathari ya uwepo wa mvua za el nino hivyo wananchi wachukue taathari mapema kabla azijaanza kunyesha Ila baada yakuanza kunyesha bado zimeleta mathara kwa wananchi na hata miundombinu ya barabara.