Matukio makubwa Ngorongoro
26 December 2023, 3:59 pm
Matukio makubwa kwa wilaya ya Ngorongoro kwa wiki mbili zilizopita na yaliyowagusa wananchi walio wengi wilayani hapa ni pamoja na ujio wa mkuu mpya wa wilaya wengi wakisubiri kuona utendaji wake wa kazi.
Na Edward Shao.
Haya hapa ni matukio manne makubwa kwa wiki mbili zilizopita.
1.Katika kipindi cha wiki mbili rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan aliwahamisha vituo vya kazi baadhi ya wakuu wa wilaya mbalimbali ambapo kwa wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Christian Sakullo akihamishw kutoka wilaya ya Misenyi na kuhamishiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Ngorongoro akichukua nafasi ya mwl Raymond Mwangwala aliyehamishiwa wilaya ya Rombo.
2.Naibu waziri wa madini Mh Stephan Kiluswa Amefanya ziara wilayani Ngorongoro na kufanya mkutano wa kusikilza na kutatua kero za wananchi wilayani hapa.
3.Tukio lingine kubwa ni uzinduzi wa shule mpya mchepuo wa kingereza ya Omom iliyoka Katika Kijiji cha Enguserosambu katibu tawala ya Ngorongoro bw Hamza H. Hamza akiwa mgeni rasmi huku akimualika mkuu wa wialaya ya Ngorongoro Kanali Wilson
4.Na tukio la mwisho wazee wa mila wa jamii ya kimasai wakiongozwa na Laigwanani Metui Shaduo walitekeleza maagizo ya katibu tawala wilaya aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa shule mpya ya Omom akiwataka wazee hao wa Mila kukaa na kutatua migogoro ya aridhi Katika vijiji vilovyo na migogoro hiyo ambapo wazee hao wamefanya ziara ya kutatua migogoro ya aridhi katika vijiji vya Olala na Arashi vilivyopo kata ya Arashi na vijiji vya Kirtalo na Oloipiri wilayani Ngorongoro.