Triple A FM

Yametimia, Arusha mjipange

6 February 2026, 8:06 am

Mchezaji wa Fountain Gate FC Elie Eldino Mokono

Na Joel Headman

Kama tulivyokueleza juzi kuhusu fununu za timu ya mpira wa miguu ya Fountain Gate ya Manyara kuhamia mkoani Arusha sasa yametimia

Utakumbuka kuwa Triple A fm ndio chombo cha kwanza cha habari kilichofichua mpango huo kabla ya leo kuwekwa hadharani Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa  Fountain Gate dakika chache zilizopita kumechapishwa taarifa kuwa sasa timu hiyo rasmi imehamishia makazi yake mkoani Arusha

Kupitia taarifa hiyo imewashukuru wakaazi wa Babati na Manyara kwa ujumla kwa kuinga mkono timu kwa muda waliyokuwa nayo huku sababu kuu ikielezwa kuwa ni kufungua fursa zaidi kibiashara na uwekezaji

Taarifa rasmi ya Fountain Gate

Mapokezi rasmi ya Fountain Gate yamepangwa kufanyika leo Feb.6 yakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Amos Makala na wana Arusha wakiombwa kujipanga kuipokea timu yao mpya