Triple A FM
Triple A FM
4 February 2026, 7:36 pm

“Timu kwakweli iendelee kubaki kwa sababu ni timbu ambayo tulishaizoea kwamba inatupa burudani ya kimpira”
Baada ya mchezo wa leo kati ya Fountain Gate na Namungo kumalizika kwa sare ya 1-1 mashabiki wa mpira wa miguu mkoani Manyara ni kama machale yamewacheza bwana.
Sasa iko hivi kuna fununu zinaenea hapa Manyara kuwa Fountain Gate wanahama mkoani Manyara kutimkia Arusha kutokana na sababu ambazo bado hazijawekwa wazi
Ingawa mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya Klabu kuthibitisha kwamba wanahama, tayari kwenye ukurasa rasmi wa Fountain Gate kumepostiwa picha jioni hii baada ya mchezo ikimuonyesha raisi wa timu hiyo Japhet Makau akigawa jezi kwa mashabibiki ikiambatana na maneno “Asante Manyara”
Kitendo hicho ambacho si cha kawaida kwa Makau kimezua wasiwasi kwa mashabiki kuwa huwenda lisemwalo lipo au kama halipo basi linakuja
Bado hakuna kauli rasmi ya klabu mpaka sasa iliyotolewa kuthibitisha fununu hizo na jitihada za kuwapata zinaendelea
Kwa upande wa mchezo waalimu wa timu zote mbili wamezungumzia matokeo hayo
Magoli ya mchezo wa leo yamefungwa na Kassim Haruna dakika ya 43 na kwa upande wa Namungu akifunga Ngoy wa Ngoy Fabrice dakika ya 69 ambaye ameibuka mchezaji bora wa mchezo