Triple A FM
Triple A FM
3 February 2026, 4:41 pm

Na Joel Headman
Serikali imekusudia kupunguza adha zinatotokana na matumizi ya bima ya afya kwenye hospitali mbalimbali ikiwemo kuondoa ubaguzi wa huduma kwa wagonjwa
Adhma hiyo imetangazwa na Waziri wa afya Mohamed Mchengerwa katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya Habari nchini kujadili juu ya ujio mpya wa bima ya afya kwa wote ambayo tayari uandikishaji umeanza kwa makundi maalum
Waziri Mchengerwa amesema serikali itatumia mbinu tofauti kuwafikia wananchi popote walipo ili kupata uelewa na ushawishi wa kuingia kwenye vifurushi vya bima mpya vyenye gharama nafuu
Serikali imeeleza kuwa kupitia bima mpya itajumuisha watu sita wa kaya moja bila kujali ni mzaliwa wa familia au lah na watapata kitita cha bima ya afya kwa shilingi 150,000/= kwa kaya zilizopo kwenye makundi maalum