Triple A FM
Triple A FM
21 January 2026, 11:13 am

Na Joel Headman
Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe ameeleza namna ambavyo chama hiko kilikuwa imara kutokana na namna kilivyojengwa
Akizungumza Tengeru mkoani Arusha kwenye msiba wa mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Mbowe amesema miongoni mwa vitu wanavyovikumbuka zaidi ni namna marehemu mtei alivyoijenga CHADEMA
Pia ameeleza kuwa Edwin Mtei ameacha uzoefu mkubwa katika vyama vya siasa nchini kutokana na autendaji wake wakati akiwa hai
Mwili wa Edwin Mtei unatarajiwa kuzikwa Jumamosi ya Januari 24, 2026 nyumbani kwake Tengeru mkoani Arusha.